Afande Sele: Simjui Kwa Sura Gigy Money Lakini Huwa Nasikia Anapenda Kukaa Uchi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Afande Sele: Simjui Kwa Sura Gigy Money Lakini Huwa Nasikia Anapenda Kukaa Uchi

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Afande Sele amesema muziki wa sasa umekuwa na mmomonyoko wa maadili kutokana na baadhi ya nyimbo zinazotoka sasa.

Mkali huyo wa rhymes katika mahojiano na Planet Bongo ya EA Radio ametaja baadhi ya wasanii ambao nyimbo zao hazina maadili ni pamoja na Msaga Sumu na Gigy Money.

“Gigy Money off course simjui hata kwa sura lakini namsikiaga kuwa ni dada ambaye anapenda kukaa uchi, anapenda kufanya vitu sijui vya aina gani huo ndio mmomonyoko wa maadili, hivyo inaonekana malezi yake hayana maadili” amesema.

“Kuna vitu vingi anavifanya vinafanya ajulikane kabla ya huo muziki alikuwa anajulikana kwa kumwaga radhi. Hao wakina Msaga Sumu ndio muziki wao wa ovyo, muziki ambao una matusi” amesisitiza.

Gigy Money anatamba na wimbo uitwayo Papa huku Msaga Sumu akitamba na ngoma ‘Mwanaume Mashine’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.