Zlatan Anasubiri Kwanza Benchi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zlatan Anasubiri Kwanza Benchi

Manchester, England.Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema, Zlatan Ibrahimovic ataanzia benchi katika mechi yao ya leo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Basel.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, alikuwa akisumbuliwa na maumivu kwa muda mrefu lakini Jumamosi iliyopita aliingia uwanjani na kuonyesha soka la maana ambapo timu yake ilimaliza kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle United. Katika mchezo huo alitokea benchi na kuchukua nafasi ya Anthony Martial.

Awali kulikuwa na minong’ono kwamba ataanza na Romelu Lukaku katika Uwanja wa St Jakob-Park, lakini Mourinho ameibuka na kusema; “Zlatan ataanzia benchi. Nitamtumia baadaye, ni mchezaji mzuri, anaweza kubadilisha matokeo saa yoyote.

“Anapokuwa uwanjani huwa anaongeza uthabiti wa kikosi.

Katika hatua nyingine huenda Henrikh Mkhitaryan akajumuishwa katika kikosi cha kwanza baada ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Newcastle wikendi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.