Spika wa Bunge Aweka Wazi Siku ya Kuapishwa Rais Mpya Zimbabwe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Spika wa Bunge Aweka Wazi Siku ya Kuapishwa Rais Mpya Zimbabwe

Robert Mugabe akiwa na Emmerson Mnangagwa

Baada ya Spika wa Bunge la nchini Zimbabwe, Jacob Mudenda Jumanne hii kutangaza kujiuzulu kwa Rais Robert Gabriel Mugabe, ameweka tena wazi siku ya kuapishwa kwa kiongozi mpya atakayekalia kiti hicho kilichoachwa wazi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ZBC la Zimbabwe, Spika Mudenda amezugumza na waandishi wa habari katika jengo la Bunge mchana huu na kusema, kwa mujibu wa katiba wa chama cha Zanu-PF kimemteua makamu wa rais wa zamani Emmerson Mnangagwa kuchukua nafasi ya Robert Mugabe kama rais wa Jamhuri ya Zimbabwe.

Spika Mudenda ameongeza, Bunge limemwambia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri, Dk Misheck Sibanda kuteuliwa kwa Mnangagwa ili afanye maandalizi ya sherehe ya kuapa kwake kama rais wa Zimbabwe.

Spika huyo amesisitiza kuwa Dr Sibanda anafanya mipango ya kuhakikisha kiapo hiko kinafanyika siku ya Ijumaa hii.

Mnangagwa anatarajiwa kuwasili leo nchini Zimbabwe ambapo atatua katika uwanja wa ndege wa Manyame Airbase uliopo mjini Harare akitokea huko alipokuwa amekimbilia baada ya kufutwa kazi na Rais Mugabe wiki mbili zilizopita.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.