Shilole: Hamna Kadi ya Mwaliko Kwenye Ndoa Yangu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole: Hamna Kadi ya Mwaliko Kwenye Ndoa Yangu


MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘ Shilole’ amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa yake Desemba, mwaka huu na mpenzi wake Ashirafu Uchebe, lakini sherehe ya ndoa wataifanyia sehemu ya wazi ili kila mtu ahudhurie, hivyo itakuwa haina kadi ya mwaliko.

Shilole ameiambia Kilinge k u w a anamshukuru Mungu, mpenzi wake huyo ameshatoa mahari kubwa nyumbani kwao, kwa hiyo kilichobaki sasa hivi ni ndoa tu na haitakuwa ya kuhudhuriwa na watu maalumu kama wanavyofanya wengine, bali k ila mmoja anaweza kuishuhudia.

“Ndoa yangu sitafanya ya siri kama wanavyofanya watu wengine, nitafanya sehemu ya wazi kabisa na wala haitakuwa na kiingilio hata kidogo, maana napenda ionwe na watu wote na washuhudie kila kin a c hoe ndelea,” alisema Shilole.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.