Nuh Afunguka Kuhusu Mwanaume Aliyemchukua Mkewe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nuh Afunguka Kuhusu Mwanaume Aliyemchukua Mkewe

Nuh Afunguka Kuhusu Mwanaume Aliyemchukua Mkewe
BAADA ya habari kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwanaume aliyemuoa aliyekuwa mke wa ndoa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, kwamba aliwahi kufanya naye kolabo na ndiye aliyemtoa kijijni kwao Iringa, mwenyewe ameibuka na kupangua taarifa hizo.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Nuh alisema kuwa, hamfahamu huyo mwanaume kama watu wanavyosema kwamba alimtoa Iringa na kuja kukaa kwake huku akifanya naye kolabo na ndipo alifahamiana na aliyekuwa mkewe Nawal.

“Simfahamu kabisa huyo mwanaume zaidi ya kumuona kwenye picha, nawaomba mashabiki wangu wasinihusishe kabisa na hao watu maana kama ni Nawal yupo na maisha yake nami niko na maisha yangu, nipo kikazi zaidi kwani kwa sasa ninatembea mikoa mbalimbali kufanya shoo wala sina habari na mtu,” alisema Nuh.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.