Mama Kanumba Amkingia Kifua Hamisa Mobetto - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mama Kanumba Amkingia Kifua Hamisa Mobetto

MAMA wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amemkingia kifua mwanadada Hamisa Mobetto, baada ya mrembo huyo kuonekana mnafiki kwa kumsikitikia muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kisha kuonekana akiwa beneti na mama huyo.

Hivi karibuni, Mobetto alionekana kwenye uzinduzi wa filamu ya Zero Player aliyoshirikiana na mdogo wa Kanumba, Seth Bosco akiwa na mama huyo ndipo watu mitandaoni walipoanza kumnanga kwa kumuita msaliti wakidai ni hivi karibuni tu, aliposti picha ya kumsikitikia Lulu aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela ambaye hapatani na mama Kanumba.

Ishu hiyo ilimuibua mama Kanumba ambapo alimtetea Mobeto: “Sioni haja ya watu kumsema vibaya Hamisa, wote ni watoto wangu tatizo liko wapi, wasimuite mnafiki bwana,” alisema mama Kanumba.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.