Huyu Ndiye Miss World Africa 2017, Magline Jeruto - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huyu Ndiye Miss World Africa 2017, Magline Jeruto

Shindano la kumsaka mrembo wa dunia (Miss World 2017) limefikia tamati wikiendi iliyopita nchini China – Sanya , huku Kenya ikiweka historia kwa kunyakuwa taji la Miss World Africa 2017 kupitia Miss Kenya 2017 Magline Jeruto (24).

Mrembo huyo alifanikiwa kuingia katika nafasi ya juu kutoka warembo 118 hadi 40 bora na kisha 10 na baadae akaingia katika nafasi ya tano bora ambapo aliwaza kuiwakilisha vyema Afrika Mashariki katika tasnia hiyo.
Magline Jeruto alitawazwa kuwa Miss Kenya Septemba 15 mwaka huu akiwa anatoka Miss Elgeyo Marakwet, mji wa Seneta Kipchumba Murkomen.
Mrembo huyo alihitimu masomo yake ya chuo mwaka 2016 mpaka anafanikiwa kuyakuwa taja hilo amekuwa akifanya kazi katika kampuni ya Lang’ata inayohusika na usafirishaji. Vile vile mrembo huyo amekuwa akijihusisha katika masuala ya Utalii.

Manushi Chhillar kutoka India aliibuka kuwa Miss World 2017, huku nafasi ya pili Andrea Meza, kutoka nchini Mexico na mrembo Stephanie Hill, kutoka Uingereza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.