Fedha Siyo Kigezo Changu cha Kutoka Kimapenzi na Mwanaume - Nandy

Akipiga stori na Risasi Vibes, Nandy ambaye anatamba na ngoma ya Kivuruge alisema anachopenda yeye ni mwanaume mcha Mungu na mchapakazi, haijalishi kama hiyo kazi inamuingizia kipato kikubwa au la.
“Fedha siyo kigezo cha mwanaume kuwa na mimi, muhimu mtu awe na hofu ya Mungu, asiwe mtu wa kujibweteka awe anajish-ughulisha kwa kazi yoyote ile, tutapambana wote kutafuta maisha hadi mambo yatakapokuwa vizuri na kujivunia kwa pamoja,”alisema.
Download App Yetu MPYA >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !
No comments
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.