Enock Bella Ajibu Aslay Kuondoka na Daftari la Nyimbo Yamoto Band - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Enock Bella Ajibu Aslay Kuondoka na Daftari la Nyimbo Yamoto Band

Kwa namna msanii Aslay anavyoachia ngoma kila wakati, mashabiki wamekuwa wakitania huenda aliondoka na daftari la nyimbo katika kundi la Yamoto Band, sasa Enock Bella amejibu kuhusu hilo.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Sauda’ amesema hapana hilo halipo ni Mwenyenzi Mungu tu kamjalia Aslay kipaji na mtunzi mzuri kitu ambacho hata yeye anakipenda.

“Unajua yote hiyo kwa sababu hakutaka promo kuwa kigezo chake kikubwa sana kwa hiyo akatumia kwa kuwepo nafasi hii anaweza akafanya vitu vingi sana, kwa hiyo anafanya kile kitu alichonacho” Bella ameiambia E Fm.

Tangu kusambaratika kwa kundi la Yamoto Band Aslay ametoa ngoma nyingin zaidi ukilinganisha na wasanii wenzake waliokuwa wakiunda kundi hilo (Bella, Beka na Maromboso).

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.