Dalili Kuu 7 Zinazoonyesha Mtu Ambaye Atachelewa Sana Kufanikiwa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dalili Kuu 7 Zinazoonyesha Mtu Ambaye Atachelewa Sana Kufanikiwa.


1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo  lakinihana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.


2. Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie, kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana MUDA wa Kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wanabahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine.Huongea sana Kuliko Kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo ? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo.

NDOTO YAKO INAWEZEKANA, CHUKUA HATUA.

DOWNLOAD APP YETU TUKUTUMIA MBINU, MAUJANJA YA MAISHA KILA TIME ''BURE KABISA'' >>BOFYA HAPA<< 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.