Baraka Da Prince Atangaza Ujio Mpya wa Bana Muziki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baraka Da Prince Atangaza Ujio Mpya wa Bana Muziki

Msanii wa muziki wa kizazi kipya cha Bongo Fleva kutoka Tanzania, Barakah The Prince ametangaza ujio wa kitu kingine ambacho ni kikubwa chini ya kivuli cha leb ya muziki inayomhusu kwa ushirikiano wake na mpenzi wake Naj, BANA MUSIC.

Akipiga stori na Dizzim online Barakah amesema kuwa ni kweli amekuwa akifanya kazi na watayarishaji na studio ambazo zinamhitaji na anazohitaji pia kulingana na ukaribu wao, lakini sasa wako katika umaliziaji wa studio za BANA na utaanza kuaandaa kazi muda wowote kuanzia sasa.

“Nimeamua sasa niliweke wazi kwasababu wengi wanaona nafanya kazi studio tofauti na wanajiuliza maswali, studio za BANA MUSIC iko katika umaliziaji na kazi soon itaanza. Kazi zenye ubora ni kikubwa tunachozingatia na naamini utayarishaji wetu unazingatia kile ambacho mashabiki wanahitaji kukisikia” Amesema Barakah The Prince.
Hata hivyo Barakah ameweka bayana kuwa mbali na kuwa miongoni mwa waanzilishi wa lebo ya BANA, wapo wasimamizi ambalo wanaisimamia lebo hiyo na muziki wake kwa ujumla katika kuhakikisha kazi zamuziki wake zinaenda na lebo inaweka mizizi ya kusonga mbele. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.