Baada ya Jux, Vanessa Mdee Atua Kwa Cassper Nyovest - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Jux, Vanessa Mdee Atua Kwa Cassper Nyovest

Cassper Nyovest ameachia ngoma yake mpya hiyo ‘Baby Girl’ ambayo Vanessa ndio kachukua nafasi hiyo ‘video queen’.

Hii si mara kwanza kwa Vanessa kufanya hivyo, utakumbuka January 2015 alitokea kwenye video ya Jux katika ngoma ‘Sisikii’, baada ya hapo waliweza kutoka ngoma ya pamoja inayokwenda kwa jina la Juu.

Hata hivyo kuna uwezekana mkubwa Cassper Nyovest akapita katika nyayo za Jux kwa kuja kuachia ngoma na Vanessa. Akizungumza na Dj Show ya Radio One Vanessa amesema kuna muendelezo wa kazi kati yake na rapper huyo.

“Ni project endelevu tumeanza kwanza na video yake ya ‘Baby Girl’ ambayo nimecheza, so next msubirie kidogo itakuja very soon” amesema Vanessa.

Unaweza kuitazama video hii hapa chini: Toa Comment Yako.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.