Amber Lulu Alewa Misifa Ya Msanii Prezzo Wa Kenya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Amber Lulu Alewa Misifa Ya Msanii Prezzo Wa Kenya.

Mwanamuziki na Video Vixen, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ amelewa na sifa anazomwagiwa na ‘mpenzi’ wake mpya, Prezoo.

Amber Lulu alisema ana furaha ya ajabu kutokana na video aliyoiachia Prezoo akimsifia kwamba anampenda, ni mzuri na ana roho nzuri, achilia mbali kuwa ameshamt-ambulisha kwa mama yake.

“Najisikia vizuri sana kusifiwa na Prezoo maana mtu ukikubalika lazima ufurahi kwa kweli, ni mtu wangu wa karibu na tuna mpango wa kufanya kazi pamoja pia, kuhusu uchumba na kutambulishwa kwa mama yake hilo kwa sasa ni siri kidogo ila siku ikifika tutaweka wazi kila kitu,” alisema Amber Lulu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.