Albamu ya 'A Boy From Tandale' ya Diamondi Kuachiwa Desemba Mwaka Huu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Albamu ya 'A Boy From Tandale' ya Diamondi Kuachiwa Desemba Mwaka Huu

Albamu ya 'A Boy From Tandale' ya Diamondi Kuachiwa Desemba Mwaka Huu
A Boy From Tandale inatoka Disemba 1 ya mwaka huu? Basi unaweza kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kuisubiri albamu hiyo kutoka kwa Diamond Platnumz.
Japo msanii huyo kutoka WCB ameonekana kufanya siri kwenye hilo, lakini Dj na mtangazaji wa The Beat1036 FM, Ellie Prohan ameonekana kupenyezewa taarifa hizo na Diamond mwenyewe.


Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka picha akiwa na msanii huyo wakati alipotembelea katika kituo hicho cha radio na kuandika ujumbe unaosomeka, “When the Persian Power Met The POWER HOUSE @diamondplatnumz 🔥🔥 #blessed #hallelujah @thebeat1036fm 💥 BIGGGGGG BANGER DROPPING 1st Dec #ABoyFromTandale #Hero !!! 😱😱.”

Taarifa hizo zinaweza zikawa na ukweli ndani yake kwa kuwa hit maker huyo wa Hallelujah aliwahi kuahidi kuachia albamu yake ndani ya mwaka huu na itawakutanisha wasanii wakubwa duniani. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.