Wema Sepetu Afunguka Madai ya Kulala Kwa Diamond 'Madale' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Afunguka Madai ya Kulala Kwa Diamond 'Madale'

Kwa mara ya kwanza baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu, mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ameanika ukweli juu ya madai mazito kuwa amekuwa akienda kulala nyumbani kwa mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva huko Madale-Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar.

Katika mahojiano na Ijumaa Wikienda juu ya skendo hiyo, Wema alisema kuwa, hakuna jambo linalomuumiza kama ishu hiyo ya kuambiwa huwa anakwenda kulala Madale kwa sababu hajawahi kufanya hivyo hata siku moja, lakini pia huko Madale, anakumbuka alishawahi kwenda wakati nyumba ndiyo kwanza inajengwa na hakuna aliyekuwa akiishi huko.

“Unajua kuna habari nyingine zinaweza kukushangaza sana. Kwenye kumbukumbu zangu Madale nilikwenda wakati nyumba inajengwa kwa sababu nilikuwa bado nipo kwenye uhusiano wa kimapenzi, lakini siku hizi za karibuni, sijawahi kukanyaga huko.

“Mimi huwa sielewi watu wanapokuwa wanazungumza hivyo vitu inakuwaje, yaani nashindwa kabisa kujua,” alisema Wema au ‘Keki ya Taifa’.

Wema aliendelea kusema kuwa, watu wakiwa wanajaribu kutengeneza maneno kama hayo ni tatizo kwa sababu zilipendwa wake huyo tayari ana uhusiano na mtu mwingine na wanaendelea na maisha yao hivyo kusambaza uvumi huo ni kumuumiza mwanamke ambaye yuko naye sasa hivi, jambo ambalo siyo zuri.

“Watu wanashindwa kuelewa kwa sasa kila mtu ana uhusiano wake hivyo kusema vitu kama hivyo ni kuharibiana uhusiano ambao unaendelea kwa hivi sasa kwa kila mmoja na hakuna kitu kibaya kama mtu kuvunja uhusiano wake kwa maneno ya kusikia ambayo hayana ukweli,” alisema Wema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.