Siri ya Bamia Inavyoweza Kuondoa Chunusi Usoni kwa Haraka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Siri ya Bamia Inavyoweza Kuondoa Chunusi Usoni kwa Haraka

WIKI hii kwenye urembo tutaongelea mboga aina ya bamia jinsi inavyotibu chunusi na kuziondoa moja kwa moja. Mbali na chunusi, pia husababisha ngozi kuteleza na kuwa nyororo.

JINSI YA KUFANYA
Chukua bamia zikatekate vipande, ziweke kwenye brenda kisha chukua limao kipande na maji kidogo, weka kwenye brenda kisha saga. Baada ya kupata mchanganyiko wako upake usoni mpaka kwenye shingo, acha kwa muda likauke kisha bandua kama unavyoondoa maski nyingine usoni.

FANYA HIVI SIKU TATU KWA WIKI ITAKUSAIDIA KUONDOA CHUNUSI
Bamia zina uwezo wa kuondoa bakteria usoni na muwasho wa aina yoyote kwenye ngozi. Kama utatumia kwa muda huo utakuwa na ngozi nzuri. Kumbuka: Usitumie tiba hii kama una tatizo la ngozi au kama una vidonda vyovyote usoni kwani itakusababishia matatizo makubwa zaidi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.