Sergio Aguero Huenda Akachezea Manchester City Dhidi ya Stoke - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sergio Aguero Huenda Akachezea Manchester City Dhidi ya Stoke

Sergio Aguero anahitaji bao moja kufikia rekodi ya ufungaji mabao Manchester City

Sergio Aguero huenda akachezeshwa mechi ya Jumamosi Ligi ya Premia dhidi ya Stoke wiki mbili baada yake kuhusika katika ajali ya barabarani, meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema.

Mshambuliaji huyo wa miaka 29 alitarajiwa kuwa nje kwa wiki kadha baada ya ajali hiyo iliyotokea Amsterdam mnamo 29 Septemba.

Lakini alirejea kwenye mazoezi kamili Alhamisi na meneja wake amesema hali yake ni nzuri.

Alipoulizwa iwapo Aguero atacheza, Guardiola amesema: "Pengine. Hajakuwa sawa 100% lakini amepata nafuu vyema sana."

Kiungo wa kati Fabian Delph huenda asicheze kutokana na tatizo misuli ya paja ingawa anafanya mazoezi.

Stoke watakuwa bila ikiungo wa kati Joe Allen aliyeumiwa akichezea Wales.

Mabeki Ryan Shawcross na Bruno Martins Indi pia huenda wasicheze kutokana na majeraha.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.