Nuh Mziwanda Amesema Kwa Sasa Hataki Kabisa Kusikia Suala la Mapenzi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nuh Mziwanda Amesema Kwa Sasa Hataki Kabisa Kusikia Suala la Mapenzi.

Msanii wa muziki Bongo, Nuh Mziwanda amesema kwa sasa hataki kabisa kusikia suala la mapenzi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Bao la Ushindi’ ameiambia FNL ya EATV kuwa kwa sasa anajielekeza zaidi katika kazi na si vinginevyo.

“Sasa hivi sipo kabisa katika suala la mapenzi, kama nina ganzi, sasa hivi na-relax kidogo nafanya kazi, yeah! wanawake wapo ila akitoea yule ambaye nahisi Mungu amenileta fresh,” amesema Nuh.

Alipoulizwa iwapo ana mipango ya kuja kuoa siku za mbeleni baada ya hivi karibauni ndoa yake kuvunjiaka alisema itatengemea kwa sababu yeye ni binadamu pia.

“Pia mimi ni mtoto wa kiume na ndoa ni jambo jema kwa hiyo siwezi kusema sitakuja kuoa kwa sababu huwezi kujua nini kitatokea mbele yangu,” amesema.

Nuh Mziwanda ambaye ana historia ya kuwa katika mahusiano na msanii Shilole mwaka huu ameachana na aliyekuwa mke wake wa ndoa ambaye pia walijaliwa kupata mtoto mmoja.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.