Nay wa Mitego Hataki Kuulizwa Kuhusu Diamond, Kisa Nini ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Hataki Kuulizwa Kuhusu Diamond, Kisa Nini ?

Moja ya maswali ambayo msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego anayakwepa kwa sasa ni kuulizwa uhusiano wake na Diamond Platnumz kwa sasa upo vipi.

Nay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’ katika mahojiano na Bongo5 hakutaka kujibu iwapo amezinguana na Diamond zaidi kueleza muimbaji huyo ndiye anapaswa kuulizwa swali hilo.

“Pata nafasi ya kuonana na Diamond na kumuuliza hili ambalo unaniuliza, sijui may be inaweza kuwa ni zamu yake kujibu, nadhani ni zamu yake”
alisema Nay wa Mitego.

Alipoulizwa iwapo kitendo cha yeye kuingilia mvutano uliokwepo kipindi cha nyuma katika mitandao ya kijamii kati ya Diamond, Alikiba na Ommy Dimpoz kulipelekea hilo alijibu;

“Mimi nadhani nipo wazi sana kwenye kitu ambacho nahisi ni sahihi kwangu haijalishi wewe ni mshikaji wangu, ninapohisi ni sahihi nitaongea, siwezi kuangali utanichukuliaje” amesema.

Nay wa Mitego na Diamond wameshatoa ngoma mbili pamoja ambazo ni Muziki Gani, Mapenzi Pesa ila ngoma zote Diamond kashirikishwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.