Nay wa Mitego Akiri Kuuza Magari Yake Yote ‘Kwa Sasa Napanda Daladala’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Akiri Kuuza Magari Yake Yote ‘Kwa Sasa Napanda Daladala’

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego, ameweka wazi sababu ya kuuza magari yake na kuonekana akipanda daladala, na kukiri kweli ameuza magari

Nay amesema ameuza magari hayo kwa sababu mbalimbali ambazo anazijua yeye, hivyo watu wasishangae wakimuona akikatisha mtaani kwa mguu na wasisite kumpa lifti kwenye magari yao.

“Kila mtu anazungumza lake ujue, lakini kama kuuza nimeuza kwa sababu zangu za msingi, nimemua kuachana na magari nipande daladala na bajaji, na hayo ndio maisha ambayo nimekulia, unajua mimi nimezaliwa kwenye maisha ya kawaida na mtaa ndio umenilea, kwa hiyo watu wasichoke kunipa lifti wakiniona, au wasishangae siku wakiniona natembea kwa mguu”, Nay wa Mitego aliiambia EATV.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa msanii huyo amefulia kiasi cha kufikia uamuzi wa kuuza magari yake, na baadhi ya nyumba ambazo alikuwa akimiliki, na kuonekana akitembea kwa bajaji kitu ambacho sio cha kawaida kwake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.