Mwana FA Ashindwa Kujizuia Kwa Lady Jaydee, Kisa Hiki Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwana FA Ashindwa Kujizuia Kwa Lady Jaydee, Kisa Hiki Hapa

Rapa Mkongwe anayetamba na ngoma ya Dume Suruali, Mwana FA ameshindwa kuvumilia na kuvunja ukimya kwa kuonyesha sapoti kwenye video ya ngoma mpya ya Mkongwe Lady Jaydee ‘I miss you’ ikiwa ni miaka takribani minne tangu fukuto la bifu lao.

Kupitia kwenye ukurasa wa Instagram Mwana FA ameweka video ya wimbo huo ambayo imeachiwa leo huku akiwataka watu kwenda kuitazama video hiyo kwenye mtandao wa You tube.
Mwana FA ameandika kwa lugha ya Kingereza akimaanisha “Video ya wimbo mpya wa Lady Jaydee ” I Miss You” hatimaye umetoka furahia karibu”...na Lady Jaydee akashukuru kwa ufupi kwa kuandika kwa lugha ya kingereza akimaanisha “Baraka nyingi”

Hata hivyo jambo hilo limeonekana kuwafurahisha mashabiki wengi wakiwepo wasanii wenzao ambao pia ni watu wao wa karibu kwa kuandika jumbe mbalimbali.

Mwanamuziki Ambwe Yessaya ameandika “Manka weee Lady Jaydee umetisha sana, nangojea siku yetu ya nyama ndio nikupe vocha…Mwana FA”

Mbunge wa Mikumi na Mkongwe wa Rap nchini Professor Jay naye ameandika “Thats True LOVE MISS U TOO Guy” @mwanafa @jidejaydee @aytanzania
Wawili hao inadaiwa kuwa vuguvugu la bifu lao lilianza mnamo 2013 na Mwanamuziki Lady Jaydee amekuwa akinukuliwa kwamba hakupendezwa na jinsi rafiki yake huyo (Mwana FA) alivyotumiwa na maadui zake kutaka kumuharibia tamasha lake.

Lady Jaydee kwa sasa ana Video Mpya inayokwenda kwa jina la ‘I miss you’ itazame hapa chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.