Msanii Future Awachefua Mashabiki Wake Las Vegas - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Msanii Future Awachefua Mashabiki Wake Las Vegas

Rapa Nayvadius Wilburn ‘Future’ kutoka nchini Marekani, amewachefua mashabiki wake mjini Las Vegas baada ya kuendelea kutangaza tamasha lake la muziki siku moja baada ya idadi kubwa ya mashabiki kupoteza maisha kwenye ukumbi.

Wiki iliyopita mashabiki 59 walipoteza maisha kutokana na kushambuliwa kwa risasi wakati wa tamasha la muziki la Route 91 Festival lililofanyika Las Vegas na watu 515 walijeruhiwa.

Siku moja baada ya tukio hilo, Future aliendelea kuonesha kuwa tamasha lake bado litaendelea bila ya kujali tukio hilo ambalo limewaacha mashabki wengi kwenye wakati mgumu, hivyo Future alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti tangazo la tamasha hilo linalojulikana kwa jina la Halloween, linalotarajiwa kufanyika Oktoba 28.

Mashabiki kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii wamedai msanii huyo mwenye umri wa miaka 33, haonyeshi machungu ya kupoteza maisha kwa mashabiki na wengine kujeruhiwa, hivyo alitakiwa kusitisha tamasha lake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.