Maswali ya Jaji Rumanyika kwa Lulu Kuhusu Kesi Inayomkabili ya Kuua Bila Kukusudia - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Maswali ya Jaji Rumanyika kwa Lulu Kuhusu Kesi Inayomkabili ya Kuua Bila Kukusudia

Maswali ya Jaji Rumanyika kwa Lulu Kuhusu Kesi Inayomkabili ya Kuua Bila Kukusudia
Baada ya Muigizaji, Elizabeth Michael ‘Lulu’kuanza kujitetea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Steven Kanumba bila kukusudia, msanii huyo amekana kuhusika na kifo hicho.

Lulu ameeleza siku ya tukio, Kanumba alikuwa amelewa na yeye Lulu alitaka kutoka na marafiki zake lakini alimkataza, baada ya Kanumba kuona simu ya Lulu imeita alizani anaongea na mwanamme mwingine huku ambapo alichukua panga na kumkimbiza nalo. Kanumba alianguka na Lulu kuchukua gari na kukimbilia Coco Beach ambapo baadaye alikamatwa na polisi maeneo ya Bamaga.


Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika amemtwanga maswali Lulu kama ifuatavyo;


Jaji Sam Rumanyika: Kipindi unaendesha gari ulikuwa na leseni halali?


Lulu: Ndiyo.


Jaji: Tufafanulie uhalali wake.


Lulu: Nilikuwa sina.


Lulu: Baada ya kukamatwa nilipelekwa kituo cha polisi Oysterbay nilikuwa nikihojiwa nikiwa sijui kama Kanumba amefariki.


Lulu ameeleza hayo leo Jumatatu akijitetea katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.