''Kikosi Cha Guardiola Kinacheza Soka Maalum'' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

''Kikosi Cha Guardiola Kinacheza Soka Maalum''

Kikosi cha Guardiola kinacheza soka maalum, kulinagan ana kipa wa zamani wa Man City

Pep Guardiola amebadilisha mchezo wa klabu ya Manchester City na sasa mchezo wa kikosi hicho umeanza kuwavutia mashabiki kote duniani kupitia ''soka maalum'' kulingana na kipa wa zamani wa klabu hiyo Shay Given.

Kikosi cha Guardiola kinaongoza ligi ya Uingereza kwa pointi tano kikiwa kimefunga mabao 35 katika mechi 10 na kupoteza pointi mbili pekee.

City ilimaliza katika nafasi ya tatu katika msimu wa kwanza chini ya ukufunzi wa raia huyo wa Uhispania na imetumia £200m kuwanunua wachezaji wapya msimu uliopita.

''Vipaji vilivyopo mbali na vile vilivyo miongoni mwa wachezaji wa ziada mara nyengine vinaziogopesha timu nyengine'', Given aliiambia BBCSport.

''Kikosi kilichoandaliwa na Guardiola kinavutia sana''.

''Amekuwa katika msimu wa kwanza na amekuwa akijifunza kuhusu kikosi chake na kukiimarisha''.

Ni vyema kuwa na vipaji , lakini la muhimu ni kuwapanga wachezaji hao na kuhakikisha kila mmoja wao anaonyesha umahiri wake na Guardiola nadhani amefanikiwa kutekeleza hilo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.