Jose Mourinho Asema Hatastaafu Akiwa Manchester United - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jose Mourinho Asema Hatastaafu Akiwa Manchester United

Manchester United walitoka sare 0-0 na Liverpool Jumamosi

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema haamini kwamba atastaafu ukufunzi akiwa bado katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia.

Mreno huyo wa miaka 54 ambaye kwa sasa anahudumu kwa msimu wake wa pili kama mkufunzi Old Trafford hajawahi kukaa zaidi ya miaka minne katika klabu moja.

Amefanya kazi katika jumla ya klabu saba.

Akiongea na runinga moja ya Ufaransa, Mourinho alisema anafikiri kwamba Paris St-Germain ni klabu nzuri sana.

"Mimi bado ni mkufunzi anayepatwa na wasiwasi, mwenye ndoto, na mwenye hamu ya kufanya mambo mapya," amesema Mourinho.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid, Inter Milan na Porto aliambia kipindi cha Telefoot cha TF1 kwamba: "Siamini, hapana, sina uhakika kwamba nitafikisha kikomo ukufunzi wangu hapa."

Alipoulizwa iwapo alikuwa anamaanisha IManchester United, Mourinho alisema: "Ndio".

Mourinho, aliyeshinda Kombe la EFL na Europa League msimu wake wa kwanza Old Trafford, amesema mtoto wake wa kiume amekuwa akitazama mechi za PSG sana karibuni.

"Kwa nini Paris? Kwa sababu kuna jambo maalum huko. Ustadi, ubora, ujana, mambo mazuri sana," aliongeza.

Mkataba wa Mourinho kwa sasa ni wa miaka mitatu na anaweza kuongezewa mkataba huo hivyo basi anaweza kusalia United hadi 2020.

Awali hata hivyo amewahi kudokeza kwamba angependa kukaa United kwa muda mrefu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.