Huddah Kuchukua Nafasi ya Vannessa kwa Jux ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huddah Kuchukua Nafasi ya Vannessa kwa Jux ?

Mwanamitindo na Mfanyabiashara kutoka Kenya, Huddah Monroe, amefunguka na kusema kwamba anadhanii Msanii Juma Jux wa Tanzania ni mwanaume ambaye yeye anaweza kuwa naye kimahusiano huku akimmwagia sifa kuwa anamuonekano mzurii kwenye mavazi.

Akifanya mahojiano maalumu na kipindi cha Nirvana kinachorusha kila Jumanne saa tatu usiku chini ya Mtangazaji Deogratius Kithama, Huddah alijibu swali la mtangazaji huyo kama anaweza kuwa kwenye mahusiano na Jux baada ya kumsifia kuwa ana muonekano wa tofauti na wenye kuvutia.

"Aaah, Nafikiri ni mwanaume ambaye naweza kuwa naye kwenye mahusiano...... Yupo 'single? hata mimi nitapatikana....." amesema Huddah.

Aidha Huddah amemshauri Jux kufanya kolabo na wasanii wakubwa zaidi wa kimataifa ili azidi kuwa msanii kubwa zaidi ndani na nje ya kimataifa kwani anamuonekano wa kuwa mtu maarufu.

Mbali na hayo Huddah amekiri kwamba alishawahi kumcheki Jux kupitia mtandao na kumwambia jinsi gani anapenda muonekano wake wa mavazi na jinsi ambavyo anavaa tofauti na jinsi jamii zinavyomfikiria.

Mtazame hapa chini Huddah akifunguka zaidi juu ya Jux.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.