Harmonize Aitazama Hallelujah ya Diamond Kama Fursa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize Aitazama Hallelujah ya Diamond Kama Fursa

Msanii wa WCB, Harmonize amesema kitendo cha yeye kuoneka katika video ya Diamond Hallelujah na ni fursa kubwa kujitangaza.

Hatmaker huyo wa ngoma Show Me hadi Shalula, amekiambia kipindi cha Clouds E kuwa si kila sehemu Diamond alipofika na muziki wake umefika, hivyo nafasi hiyo ni kubwa kwake.

“Kuonekana kwenye video ya msanii kama Diamond ni credit kwangu kwa sababu ni video ambayo ni international inaenda mbali, siyo kila sehemu anayofika Diamond na mimi nafika” amesema Harmonize.

“Kuna sehemu watu hawanijui na kuna sehemu nyingine nimefika kupitia Diamond kwa hiyo ile ni fursa kwangu mimi kwa sababu itafika sehemu ambayo muziki wangu haujafika, sidhani kama nitakuwa nimefika Jamaica” ameongeza.

Katika ngoma hiyo ambayo Diamond amewashirikisha Morgan Heritage si Harmonize pekee yake aliyeonekana bali hata Rich Mavoko, video ilifanyika nchini Uingereza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.