Hamisa: Sina Tatizo Na Zari wa Diamond - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hamisa: Sina Tatizo Na Zari wa Diamond

Mrembo Hamisa Mobetto amesema hana tatizo lolote na mpenzi wa Diamond, Zarina Hassan na anaamini siku moja watakuwa sawa.
 
Hamisa amesema hayo jana Ijumaa wakati wa sherehe maalum aliyoandaa kwa ajili ya mtoto wake Abdul Nassib.
 
Amesema licha ya kuwepo kwa maneno na hali ya kutoelewana kwa sasa anaamini utafika wakati watakuwa pamoja.
 
"Watoto wameshatuunganisha, najua kwa sasa mambo na maneno ya watu ni mengi ila ipo siku kwa sababu mtoto wangu ana ndugu na watoto wake basi tutakuwa sawa tu.Maana inawezekana mtoto wangu akataka kuwatembelea ndugu zake au wale wakamtaka ndugu yao kwa hiyo yote yanawekezekana," amesema

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.