Gigy Money Ataja Dau la ‘Papa’ Kwa Yeyote Anayemuhitaji - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money Ataja Dau la ‘Papa’ Kwa Yeyote Anayemuhitaji

Msanii wa Bongo Fleva na Video Queen, Gigy Money amesema kwa sasa kama promota au mtu yeyote anayehitaji kumuita kutumbuiza kwenye tamasha/sherehe yake basi ni lazima uwe na kiasi cha milioni mbili za kitanzania.

Mkali huyo anayetamba kwa sasa na wimbo wake wa ‘Papa’ amesema wimbo huo ni ‘Hit Song’ na ni moja ya wimbo mkali kwa sasa kuliko nyimbo nyingine zilizotoka kwa muda huu.

“Na-perform stejini kwa milioni mbili, Papa is a hit song, bila milioni 2 siwezi kutoa Papa stejini, is a hit song.“amesema Gigy Money kwenye mahojiano yake na Bongo5.

Hata hivyo, Gigy Money amesema kwa sasa wimbo huo unamfanya afikirie jinsi gani atarudi na ngoma nyingine kali zaidi ya Papa.

- Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.