Fellaini Kukosa Mechi na Liverpool Kutokana na Jeraha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Fellaini Kukosa Mechi na Liverpool Kutokana na Jeraha

Fellaini kukosa mechi na Liverpool kutokana na jeraha.

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United, Marouane Fellaini huenda akakosa mechi ya Premier League huko Liverpool kufuatia jeraha la mguu.

Fellaini 29, aliondoka uwanjani baada ya dakika 29 wakati wa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Bosnia-Herzegovina siku ya Jumamosi.

Raia huyo wa Ubelgiji aliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa alifanyiwa uchunguzi na huenda akakos kucheza kwa wiki kadhaa.

Watakutana na Cyprus wakati wa mechi yao ya mwisho ya kufuzu siku ya Jumanne, huku United ikisafiri kweda Anfield tare 14 Oktoba.

Fellaini ameifungia Manchester mabao manne msimu huu ukiwemo ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Crystal Palace.

Anaungana na mchezaji mwenaake Paul Pogba ambaye yuko nje kufuatia jeraha la msuli.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.