Anthony Joshua: Mwaka 2018 Utaanza Vizuri Kwangu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Anthony Joshua: Mwaka 2018 Utaanza Vizuri Kwangu

Joshua akiwa na baba yake baada ya kumchapa Carlos Takam

Bondia Anthony Joshua amesema upo uwezekano wa mwaka 2018 kuanza vizuri baada kumaliza 2017 kwa kumchapa Carlos Takam.

Joshua bingwa wa uzito wa juu wa taji la WBA na IBF aliendeleza ushindi wake alioupata mwezi April dhidi ya Wladimir Klitschko kwa kumchapa Takam ndani ya raundi 10 mjini Cardiff.
Mwamuzi alimaliza mchezo huo baada ya kuona Takam akishambuliwa kwa makonde mfululizo

Mdhamini wake Eddie Hearn amesema kuna uwezekano akachauana na Deontay Wilder huku kocha wake Rob McCracken akimtaja Joseph Parker kuwa anafaa zaidi.

Antony Joshua amekuwa miongoni mwa wanamichezo wanaovutia zaidi kwa siku za karibuni, huku akiweka rekodi ya kushinda kwa asilimia mia moja kwenye michuano yake yote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.