Alikiba na Mchumba Wake Kimenuka Haswaa ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba na Mchumba Wake Kimenuka Haswaa !

MKALI anayetamba na wimbo wa Seduce Me, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ amedaiwa kuingia kwenye mgogoro na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Amina Khaleef.

Kwa mujibu wa chanzo, Kiba na mchumba huyo ambaye wana malengo ya mbali, walizinguna baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa picha zinazomuonesha staa huyo akiwa na mrembo aitwaye Carlo jijini Mwanza.

“Yani nakwambia kimenuka, unajua yeye (Amina) yule si unajua anaishi Mombasa sasa akiona tu picha kwenye mitandao huwa ni ngumu sana kuelewa kama ni uzushi.

“Ishu ilifahamika kabisa kwamba haina ukweli wowote lakini kwa mchumbake mambo yalikuwa tofauti. Amegoma kabisa kuelewa,”
kilivujisha mchapo huo chanzo chetu cha uhakika.

Amani lilimvutia waya Kiba ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo, simu yake iliita bila kupokelewa. Hata hivyo, alipopigiwa mmoja wa maneja wake ambaye aliomba hifadhi ya jina, alikiri kutokea kwa tafrani hiyo lakini akasema ni mambo ya kawaida hivyo wanaweza kulimaliza.

“Si unajua kwenye uhusiano vitu kama hivyo ni vya kawaida, huwa yanatokea mara kwa mara na wana-solve hivyo hata hili naamini litapita.

“Ni kama vile mimi na wewe inavyotokea hata wao pia inatokea, ni mambo ya kawaida,” alisema meneja huyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.