Afya:Vitambue Virusi Vienezwavyo Kwa Busu La Mdomoni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Afya:Vitambue Virusi Vienezwavyo Kwa Busu La Mdomoni
Utafiti uliochapishwa na jarida la Microbiome la Uingereza limeonyesha kuwa upigaji busu unaweza kusafirisha zaidi ya bakteria milioni80 kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Daktari Sophianis Nyomyani wa Hospitali ya Mwananyamala anazungumzia utafiti huo na kusema  bakteria wengi ambao huambukizwa kwa njia ya busu na wengi huchukulia busu kama njia pekee ya kuonyesha upendo.

Utafiti huo pia umesema wapenzi ambao hupigana mabusu kwa wastani wa mara tisa kwa siku huwa na bakteria ambao wanaendana na hubadilishana kila wanapofanya tendo hilo.

“Ni upendo ila kiafya si salama,hata kama wanandoa wanashiriki katika kupigana busu,isiwe kwa kila mtu,ni lazima kuwe na mipaka,unaweza kumbusu mtu shavuni,nje ya mdomo,mkononi na kwingineko lakini siyo lazima mdomoni.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.