Samatta, Msuva, Banda, Waing'arisha Tanzania - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Samatta, Msuva, Banda, Waing'arisha Tanzania

Wachezaji wa Kimataifa wa Tanzania mshambuliaji Mbwana Samatta, Simon Msuva na Abdi Banda wamefanya vizuri na vilabu vyao katika michezo ya katikati ya wiki.

Mbwana Samatta akiwa na KRC Genk ya Ubeligji wamefanikiwa kusonga mbele kwenye kombe la Ubelgji baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Cercle Brugge Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge usiku wa kuamkia leo. Katika mchezo huo Samatta amecheza dakika 75.

Naye Mlinzi wa zamani wa Simba Abdi Banda akiwa na timu yake ya Baroka FC wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Bloemfontein Celtic katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Banda akicheza dakika 90.

Wakati huo Simon Msuva usiku wa jana ameisaidia timu yake Difaa Hassan El-Jadida kusonga mbele katika Kombe la FA Morocco baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Ittihad Tanger Uwanja wa Grand Stade de Tanger. Msuva amecheza dakika zote 90 na kutoa mchango mkubwa kwenye ushindi huo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.