Rich Mavoko Afunguka Baada ya Diamond ‘Kukinukisha’ Kwenye Fresh Remix - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rich Mavoko Afunguka Baada ya Diamond ‘Kukinukisha’ Kwenye Fresh Remix

Msanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Rich Mavoko ametoa mtazamo wake baada ya watu wengi kumtupia maneno Fid Q kwa kile walichodai amemruhusu Diamond kutupa vijembe kwa Alikiba kupitia ngoma yake ‘Fresh Remix’

August 21, 2017 Fid Q alitoa remix ya ngoma yake Fresh ambayo aliwashirikisha Diamond na Rayvanny ambapo siku kadhaa mbele Fid Q alikiri kusakamwa vilivyo katika mitandao ya kijamii. Kupitia Nipe Tano ya TBC Fm Rich Mavoko amesema;

“Kwangu mimi its easy kwa sababu hakuna muziki unaokwenda bila majibishano, hata mpira wenyewe kuna mabishano ndio maana kuna mtu kama Haji Manara. Kuna watu wanaongea sana, hivi vitu ndio vinaleta chachu ya muziki, kwa sababu hiyo mitandao yao ndio inafanya watu wanakua , kwa hiyo mimi naona kawaida tu,” amesema.

Rich Mavoko ameshatoa ngoma na Fid Q inayokwenda kwa jina la Sheri.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.