Rais Uhuru Kenyatta 'Naheshimu Maamuzi ya Mahakama' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rais Uhuru Kenyatta 'Naheshimu Maamuzi ya Mahakama'

Baada ya Mahakama ya juu nchini Kenya kutengua matokeo ya Uchaguzi nchini humo, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amezungumza kwa mara ya kwanzajuu ya maamuzi hayo na kusema yuko tayari kurejea kwenye ulingo wa kutetea nafasi kwa marudiano huku akisisitiza amani itawale.

Akiwa ameambatana na makamu wake, William Ruto, Kenyatta amesema amekubali uamuzi wa Mahakama licha ya kwamba hajaafikiani na Majaji sita waliohusika kutoa maamuzi hayo.

Kenyatta amesema haiwezekani raia zaidi ya milioni 40 wa Kenya waliochagua chama chake cha Jubilee, maamuzi yao yaje yatenguliwe na watu sita.

“Tuko tayari kurudi tena kwa wananchi, tukiwa na ajenda ile ile tuliyowasilisha, ajenda ya kuunganisha nchi. Kuunda chama cha taifa. Kuendeleza nchi hii, hatuko kwenye vita na ndugu zetu wa upinzani….tuko tayari kurudi kwa debe, kuongea na Wakenya, kuwaambia yale tunataka na yale tunataka kutenda, watu sita, hawawezi kubadilisha nia ya Wakenya milioni 40, Wakenya ndio wataamua, na hivyo ndivyo demokrasia ilivyo.“amesema Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa taifa.

Hata hivyo, Rais Kenyatta amewataka wananchi wa Kenya kuendelea kuwa wamoja na kutokaribisha tofauti zao, akisema umoja ndiyo nguzo muhimu kwa taifa hilo.

“Jirani yako atasalia kuwa jirani, bila kujali mrengo wao wa kisiasa, dini, au rangi, naomba tuendelee kuwa wamoja,” amesema Kenyatta huku akisisitiza kwa kusema, “amani, amani, amani“.

Mahakama ya Juu nchini Kenya imetengua matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8 mwaka huu ambao ulimpa ushindi Rais Kenyatta kwa kusema ulikuwa na dosari, na uchaguzi utarudiwa kwa mara ya pili ndani ya siku 60.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.