Odinga Akataa Kurudiwa Kwa Uchaguzi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Odinga Akataa Kurudiwa Kwa Uchaguzi

Mgombea wa Urais nchini Kenya kupitia Muungano wa vyama vya upinzani (NASA) Raila Odinga, ameipinga tarehe ya uchaguzi iliyotolewa na Tume huru ya Uchaguzi nchini humo IEBC.

Akizungumza mchana wa leo Raila Odinga ametaka uchaguzi huo ufanyike Oktoba 24, na mitihani ya wanafunzi ya kuhitimu elimu ya msingi na sekondari ambayo wanatarajia kuifanya isogezwe mbele.

Raila Odinga aliendelea kusema kwamba IEBC ilikubaliana kukutana na NASA na Jubilee ili kupanga suala hilo, lakini tume hiyo imeamua kufanya uamuzi na Katibu wa Baraza la Elimu Fred Matiang'i, ambaye aliomba ifanyike hivyo.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika baada ya Mahakama kufuta uchaguzi wa Urais uliofanyika Agosti 8.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.