Nay wa Mitego: Napendwa Kuliko Wanaosema Kuwa Sifanyi Hip Hop - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego: Napendwa Kuliko Wanaosema Kuwa Sifanyi Hip Hop

Msanii wa muziki wa Bongo, Nay wa Mitego wamejitapa na kujivunia style yake ya muziki anayofanya licha ya baadhi ya wasanii wenzake kumuondoa katika kundi la wasanii wa hip hop.

Nay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuondolewa katika kundi la muziki wa hip hop hakumuumizi kwani anaangalia biashara na wasanii wanatakiwa washindane katika eneo hilo.

“Muziki wa hip hop unahitaji vitu ambavyo vinaishi, tuzungumzie maisha ya watu ya kila siku. Utaona wanasema Nay siyo mwanahip hop, wananitoaga kwenye kundi la hip hop lakini why ndio na mashabiki wengi kuliko wao, why nimekuwa napendwa kuliko wao, why angalau na vijihatua kuliko wao?” amesema Nay.

“Ni kwa sababu nafanya kitu cha Watanzania nafanya kitu ambacho kipo kwa wakati huo na ndivyo tunatakiwa kufanya ili isionekane kila siku waimbaji ndio wana mkwanja, tushindane. Marekani wasanii wenye hela nyingi ni wanahip hop kwanini na sisi tusiweze hivyo,”
ameongeza.

Kwa mwaka huu Nay wa Mitego ametoa ngoma kama Wapo na Moto ambazo zipo katika style ya rap, huku ngoma kama Makuzi na Acheze zikiwa katika style ya kuimba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.