Nay wa Mitego Adai ‘Upepo’ wa Diamond na Alikiba Haumzuii Kutoa Ngoma - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Adai ‘Upepo’ wa Diamond na Alikiba Haumzuii Kutoa Ngoma

Msanii wa Bongo Flava, Nay wa Mitego amesema kitendo cha wasanii wakubwa kama Diamond na Alikiba kuachia ngoma zao kipindi hiki hukumzui yeye kuachia ngoma iwapo anataka kufanya hivyo.

Hapo jana Nay wa Mitego aliachia ngoma mpya ‘Makuzi’ zikiwa ni wiki mbili tu zimepita tangu alipotoa wimbo mwingine ambao alimshirikisha Rich Mavoko.

Kupitia Dj Show ya Radio One Nay amesema akiwa na ngoma huwa haangalii ni kitu gani kinatrend kwa wakati huo.

“Watu wanaogopa kutoa nyimbo kwa sababu ya vungu vungu hili, kwangu huwa naona ni vitu ambavyo huwa vinapita haraka sana na huwa siviweki katika akili, ndio maana nikiwa na kitu changu ambacho nahisi kwa wakati huo kinatikiwa kwenda bila kuangalia kuna nini kinaendelea huwa natoa,” amesema.

“Muziki wangu una nguvu kuliko vitu vingine, mashabiki wangu ambao wanaamini kwenye kile ambacho nakifanya, so kelele za watu au purukushani za huko na kule hazinizui nikiwa na kitu changu nataka kukifanya,” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.