Mh Lazaro Nyalandu Atua Kenya Kumjulia Hali Tundu Lissu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mh Lazaro Nyalandu Atua Kenya Kumjulia Hali Tundu Lissu

Mh Nyalandu akiwa nchini, Kenya

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametua nchini Kenya Jumamosi hii kwaajili ya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliyelazwa nchini humo kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi.

Lissu wiki moja iliyopita alishambuliswa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma muda mfupi baada ya kutoka bungeni.

Ngalandu ni Mbunge wa kwanza wa CCM kufika hospitalini hapo kwaajili ya kumtakia hali mbunge huyo machachari wa Chadema.

“Nimefika Hospitali ya Nairobi mapema leo kumjulia hali Mh. Tundu Lissu. MADAKTARI wanaendelea kumfanyia matibabu, na bado hatujaruhusiwa kumuona. Kwa niaba ya wana Singida, na Watanzania wote, nimetoa salaam za pole kwa mke wake, na bado nasubiri uwezekano wa kuweza kuonana naye usiku wa leo endapo MADAKTARI wataruhusu. Cha muhimu zaidi, SOTE tuendelee KUMWOMBEA. MUNGU amtendee wema, na kumponya katika majira haya ya kujaribiwa kwake. Katika yote ndani ya yote, IKAWE HERI KWAKE. (Pichani na mdogowangu Peter Nyalandu, The Nairobi Hospital, Kenya),”
Nyalandu aliandika ujumbe huo akiwa hospitali hapo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimetolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya mbunge huyo inaendelea vizuri.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.