Mcheza Tenesi Serena Williams Ajifungua Mtoto wa Kike - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mcheza Tenesi Serena Williams Ajifungua Mtoto wa Kike

Bingwa wa tennis kwa upande bi Serena Williams amejifungua mtoto wa kike katika hospitali moja ya mjini Florida Marekani.

Japo mwenyewe na jamaa zake hawajatoa tangazo rasmi tayari kuna ujumbe wa kumpa hongera katika ukurasa rasmi wa Twitter akaunti ya US Open Tennis kutoka kwa kocha wake miongoni mwa wengine.

Itakumbukwa mwanamama huyo aliweka rekodi ya kushinda kinyanganyiro cha Australian Grand Slam kwa mara ya 23 mwaka huu January, japo alishindana akiwa mja mzito.

Serena alikiri kwamba alifichua kuhusu mimba yake kwa ulimwengu kimkosa mnamo mwezi Aprili baada ya kupakia picha katika Intagram kimakosa katika mtandao wa Snapchat.

Alishinda taji la Australian Open mnamo mwezi Januari akiwa mjamzito na katika taarifa yake katika jarida la Vogue mwezi uliopita alisema kuwa anataka kutetea taji hilo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.