Mbasha Afunguka Madai Ya Kutelekeza Watoto - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mbasha Afunguka Madai Ya Kutelekeza Watoto

Msanii wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha amesema tuhuma anazopewa na wanawake mbalimbali aliozaa nao za kutelekeza watoto siyo za kweli.

Mbasha amesema tuhuma hizo ni uongo na anachukia watu wanaotengeneza habari hizo na kusema kuwa yeye hapendi kwani watu wenye stori za namna hiyo ni wasanii wa bongo fleva.

“Sio kweli hivyo vitu ni vya uongo nakanusha kabisa hivi kwa nini vitu vingi vinaongelewa vya uongo! alafu mimi sipendi, huu uongo uongo ni vitu vya bongo fleva, mimi sipo kwenye kutafuta kiki wala kuongelea vitu ambavyo havina faida” amesema Emmanuel Mbasha.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za Mbasha kuwazalisha wanawake wawili tofauti na kuwatelekeza.

PAKUA APP YA BONGOSWAGGZ SASA UPATE UBUYU ZAIDI YA HUU KILA TIME KWENYE SIMU YAKO, >BOFYA HAPA<

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.