Mambo 5 Anayofanya Neymar Kabla Hajaingia Uwanjani Kucheza Mechi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mambo 5 Anayofanya Neymar Kabla Hajaingia Uwanjani Kucheza Mechi

Staa wa PSG Neymar anasema mambo matano anayofanya kabla ya mechi “Neymar Jr Five” Ni

1) Kuongea na Baba Yake Mzazi


Neymar ana mahusiano mazuri na baba yake,Baba yake ana nafasi kubwa kwenye maswala ya pesa ya Neymar, baba yake huchukua nafasi ya Agent wake kwenye dili tofauti kama dili ya kuhamia PSG akitokea Barcelona.

Neymar anasema “I always call my father, to talk before the game”, said the player.

2) Anasikiliza Muziki

Wanamichezo wengi husikiliza muziki kabla ya kufanya mashindano yao, Neymar hufanya hivyo kabla ya game zake zote.

3) Hufanya Maombi.

Neymar hufanya maombi mafupi kabla ya kila mchezo na hata akifunga hushangilia kwa kunyoosha vidole juu kama ishara ya kumshukuru Mungu.

4) Huenda Msalani

Neymar anahakikisha yuko tayari kwa Game muda unapofika, lazima amalize haja zake kabla hajaingia uwanjani.

5) Kupiga picha Moja

Ili kuwa karibu na mashabiki, Neymar anapiga picha moja kabla ya game zake , kama wanavyofanya wachezaji kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ilikuhakikisha followers wao kwenye mitandao kama Twitter ,Facebook na Instagram wanajua kinachoendelea.

Neymar amechangamka sana kwenye maswala ya mitandao ya kijamii.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.