Lionel Messi Afunga 4 La Liga, Zaza Apiga Hat Trick - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lionel Messi Afunga 4 La Liga, Zaza Apiga Hat Trick

Kiungo wa Barcelona Lionel Messi amefunga mabao manne katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Eibar huku Valencia nao wakiikung’uta Malaga mabao 5-0.

Messi alianza kufunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 20.

Kabla hajafunga la pili katika dakika ya 59 Paulinho na Denis Suarez walifumania nyavu za Eibar katika dakika ya 38 na 53. Mengine alifunga katika dakika 62 na 87 katika mchezo huo uliochezwa Nou Camp.

Simone Zaza alifunga hat trick katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Malaga akifumania nyavu katika dakika ya 55, 60 na 63 huku mengine yakifungwa na Santi Mina katika dakika ya 17 na Rodrigo katika dakika ya 86.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.