Kim Kardashian na Kanye West Kupata Mtoto wa 3 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kim Kardashian na Kanye West Kupata Mtoto wa 3

Kim Kardashian na Kanye West kupata mtoto wa 3

Kim Kardashian West na mumewe Kanye West wamethibitisha kwamba watapata mtoto mwengine kutoka kwa mama anayebeba mimba kwa niaba yao.

Mwisho wa kipindi chao cha The Kardishians, nyota huyo alimwambia dadake Khloe , ''Tumepata mtoto''.

Kumekuwa na ripoti nchini Marekani kwamba dadake mdogo Kim , Khloe pamoja na dada wa kambo Kylie Jenner pia ni wajawazito.

Hatahivyo mazungumzo yao hayakuangazia uja uzito wao.
Kylie Jenner kulia

Kim ambaye ameolewa na rappa Kanye West amekuwa akizungumza katika kipindi hicho kuhusu matatizo aliyonayo kushika mimba.

''Baadaya ya kuzungumza na Kanye na nadhani nilijua kwamba kupata mwanamke atakayebeba mimba kwa niaba yetu ndio lilikuwa suluhisho na hilo sasa nimeona kwamba ndio chaguo'', alisema.

Ametaja ripoti za awali kwamba amekuwa akisubiri kuwa na mtoto kutoka kwa mama atakayebeba mimba kwa niaba yake kama uongo.
Kim Kardashian na wanawe wawili

Mnamo mwezi Juni, wanandoa hao walidaiwa kukodisha mwanamke atakayebeba uja uzito kwa niaba yao kutokana na matatizo ya kiafya yaliotokana na watoto wawili wa Kim Kardishian.

Iwapo itathibitishwa atakuwa mtoto wao wa tatu baada ya North, Four na Saint ambaye atakuwa na miaka miwili mwezi Disemba.

Ripoti kadhaa za habari wiki iliopita zimesema kuwa Khloe kardashian , 33 na Kylie Jenner 20 ni waja wazito.

Hata hivyo wawili hao hawajathibitisha ama hata kukana ripoti hizo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.