Kikosi cha Arsenal Sio Cha Mchezomchezo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kikosi cha Arsenal Sio Cha Mchezomchezo

London, England. Kikosi cha Arsenal kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cologne katika mashindano ya makundi Ligi ya Europa, huku Alexis Sanchez akionyesha uwezo baada ya kufunga bao la pili na kumtoa kimasomaso Kocha Arsene Wenger kwenye dimba la Emirates.

Sanchez ambaye amekuwa kwenye hali kutengwa kutokana na kuonyesha nia ya kuhamia Manchester City wakati wa dirisha la usajili wa kiangazi siku ya kufungwa dirisha hilo, alidhihirisha ubora wake kwenye mechi hiyo ya jana Alhamisi.

Kikosi cha Cologne kilikuwa cha kwanza kupata bao la kuongoza kwenye mchezo huo kupitia kwa msahmbuliaji wake, Jhon Cordoba baada ya kumtungua kipa David Ospina.

Bao la Arsenal lilisawazishwa na beki Sead Kolasinac, huku Bellerin akifunga bao la tatu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.