Jacquline Wolper: Hakuna wa Kumuamini Kwenye Mapenzi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jacquline Wolper: Hakuna wa Kumuamini Kwenye Mapenzi

Jacquline Wolper: Hakuna wa kumwamini
Muigizaji wa filamu na Mfanyabiashara, Jacquline Wolper amefunguka na kusema iwapo mpenzi wake wa sasa (Brown) akimtenda na kumuumiza kama waliopita ataamini kuwa hakuna wa kumwamini kwenye mapenzi na kwamba wanaume wote wana matendo ya kufanana.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Wolper ambaye miezi michache alitangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake (Msanii wa muziki) ma kisha kuweka wazi mahusiano yake na Mwanamitindo Brown amesema kutokana na kijana huyo pamoja na familia yake kuwa na imani ya dini anaamini hataweza kumuumiza ingawa binadamu wana mapungufu.

"Siamini kama BFF anaweza kunifanyia vitendo vibaya kama nilivyowahi kufanyiwa. Namuamini sana kutokana na kuwa na hofu ya Mungu lakini bado sisi ni binadamu. Anaweza kunikosea kawaida au mimi nikamkosea kwa sababu sisi ni binadamu hiyo haitafanya nimchyukie lakini akifika huku pa kunifanya niumie kama nilikotoka nitaamini kuwa hakuna wa kumuamini," Wolper.

Wolper amesema kuwa, Brown ni aina ya mwanaume ambaye alikuwa akimuhitaji katika maisha yake na hatimaye Mungu kasikia kilio chake.


KUNA BONGE LA STORI KUHUSU STAR WAKO UNAYEMPENDA
>> IPO HAPA/BOFYA HAPA <<

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.