Gigy Money Atoboa Siri Ya Wimbo Wake ‘Papa’ Kufanya Vizuri - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money Atoboa Siri Ya Wimbo Wake ‘Papa’ Kufanya Vizuri

Msanii wa kizazi kipya Gift, maarufu kama Gigy Money amefunguka na kusema wasichana wapunguze kuimba maneno magumu na kutumia vingereza lugha ambazo hazieleweki na watu wote katika muziki kunawafelisha ndio maana inawawia vigumu muziki wao kuwafikia watu wa rika lote.

Gigy alizungumza hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya wimbo wake mpya unaofanya vizuri unaoenda kwa jina la Papa.

“Nitoe ushauri kwa wasichana ambao wanaimba, unajua wasichana wengi wana vipaji vya kuimba lakini wanafeli. Ukishajijua huwezi kuimba acha kuimba vitu vingi, huna uwezo wa kuimba alafu mambo unayoimba mlolongo kibao, vingereza, sijui nini utajikuta unafeli. Sasa neno kama ‘papa’ lipo uswahilini, rahisi kwa watu kuelewa”, amesema Gigy Money.

Gigy ameeleza kuwa lengo lakutoa wimbo huo wenye lugha nyepesi ilikuwa ni kuwafikia watu wenye rika lote, na anaamini kwa asilimia kubwa amefanikiwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.