Diamond Platnumz Akiri Mtoto Wa Mobetto Ni Wa Kwake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Platnumz Akiri Mtoto Wa Mobetto Ni Wa Kwake

Msanii wa kizazi kipya, Diamond Platinumz amekiri kuwa ni kweli mtoto wa Video Queen, Hamisa Mobetto ni wa kwake na alikubali kwa masharti ya kuwa Mobetto amheshimu mwanamke wake wa sasa, Zari.

Diamond amefunguka hayo leo katika mahojiano na Clouds FM katika kipindi cha Leo Tena kilichorushwa ‘live’ pia katika Clouds TV na Instagram.

Amesema kuwa Zari anafahamu kila kitu kuhusu suala hilo na hana shida yoyote lakini anashangazwa na hatua za Mobetto kujitangaza kwa lengo la kumuumiza Zari.

Akizungumzia picha na vipande vya video vilivyosambaa hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, amesema ni mpango mkakati mahususi wa Mobetto kutaka kumvuruga Diamond na Zari ili siku moja Zaria toke kwenye picha kasha yeye ndiye awe namba moja.

“Katika maisha hivi vitu vinatokea, lakini jambo muhimu ni namna gani mtu unadili na suala kama hilo kama mwanaume. Hakuna sababu ya kutengeneza vita isiyokuwa na sababu ili hata hapo baadae watoto wote waje kukua pamoja na kufurahi kama familia,” amesema.

Amedai kuwa sio kweli kwamba alikuwa na mpango wa kukataa damu yake kama ambavyo ilikuwa inasambazwa katika mitandao ya kijamii na ni kitu ambacho hawezi kufanya ndio maana amesimama kama mwanaume ili damu yake isipotee.

PAKUA APP YA BONGOSWAGGZ SASA UPATE UBUYU ZAIDI YA HUU KILA TIME KWENYE SIMU YAKO, >BOFYA HAPA<

“Nilifanya kila kitu ambacho mwanaume anapaswa kufanya, ikiwa ni pamoja na kumpatia Mobetto Shilingi elfu 70 kila siku na kumnunulia gari aina ya Rav 4 mpya kwa ajili ya kuendea kliniki na safari za mtoto za hapa na pale,” amefunguka Diamond.

Aidha, ameomba radhi kwa mama na ndugu zake kwa kuhusishwa katika vita ya maneno na matusi katika mitandao ya kijamii kwa kosa ambalo yeye mwenyewe ndiye mhusika mkuu kwasababu wakati mtoto alipozaliwa alilazimika kumuomba mama yake na ndugu zake kwenda hospitali kumuona kwa kuwa yeye alikuwa nchini Uingereza, na kwamba kama angekuwepo nchini basi angeenda hospitali mwenyewe.

“Nilimuomba mama na ndugu zangu wakamuone mtoto, lakini upande wa pili ukatumia vibaya kitendo hicho kwa kuwapiga picha na kusambaza katika mitandao ya kijamii ili ionekane kuwa wanaunga mkono jambo hilo ili tu kumuumiza mama watoto wangu Zari,” ameongeza Diamond.

PAKUA APP YA BONGOSWAGGZ SASA UPATE UBUYU ZAIDI YA HUU KILA TIME KWENYE SIMU YAKO, >BOFYA HAPA<

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.