Alikiba: ‘Seduce Me’ Haijatamba Kwa Kiki ya Ushindani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba: ‘Seduce Me’ Haijatamba Kwa Kiki ya Ushindani

Msanii Ali Kiba amesema kuwa wimbo wake wa ‘Seduce Me’ hauja tamba kwa sababu ya kuwepo kwa ushindani na wimbo wa WCB uitwao Zilipendwa.

King Kiba amesema kuwa wimbo wa Seduce Me umetamba na kupata mapokeo makubwa kutokana na ubora wa wimbo wenyewe na sio kama baadhi ya mashabiki wanao sema kuwa wimbo umetamba kutokana na kuwepo kwa ushindani wa wimbo huo na wimbo wa ‘Zilipendwa’ kutoka kwa wasafi.

‘’Seduce Me, ni wimbo ambao umetamba kutokana na nguvu kubwa ya kupokelewa na mashabiki na huo ushindani wanao uzungumzia wa wimbo wangu na huo wimbo mwingine sio kweli kwa sababu mi nafanya muziki wangu wa aina yangu’’ amesema Ali kiba

Hata Hivyo, nyimbo hizi mbili zimekuwa zikikimbizana katika chati mbali mbali za Radio na Runinga na kuwa na watazamaji wengi zaidi katika mtandao wa Youtube kuliko Video zote zilizotoka hivi karibuni hapa nchini.

Wimbo wa Seduce Me bado umezidi kuwa gumzo na kuonyesha dalili ya kuendelea kusikilizwa na kupendwa kwa muda mrefu zaidi.

UNAJUA DIAMOND AMESEMA NINI KUHUSU MTOTO WAKE NA HAMISA MOBETTO ? >BOFYA HAPA< KUPATA ZOOTE HIZI KWENYE APP YETU.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.